Thursday, 18 January 2018

Ugonjwa wa Kipindupindu



 Kipindupindu ni miongoni mwa magonjwa ambayo husababishwa na aina ya bakteria aitwaye Vibrio cholerae, bacteria huyu husababisha mtu kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya mchele. Ugonjwa huu ni wa kuambukizwa kwa njia ya viini vinavyoenezwa kupitia maji yaliyo changanyika na  kinyesi au matapishi kutoka kwa wagonjwa wenye Kipindupindu. Mlundikano wa taka na maji machafu ni moingoni mwa vyanzo vya maambukizi ya Kipindupindu.


Mlundikano wa Taka kwenye maeneo ya wapita njia

Aidha matumizi ya choo yasiyo sahihi pia huchangia maambukizi ya ugonjwa huu. Kwa mujibu wa taarifa za ya idara ya huduma za Afya na usafi wa mazingira Wizara ya Afya kipindupindu huenea kwa njia kuu sita:
1: kutokunawa mikono kwa maji safi na salama yanayotiririka na sabuni kabla ya kula au baada ya kutoka chooni.
2:kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salama.
3: kunywa maji yasiyosafi na salama.
4:kumhudumia mgonjwa mwenye dalili za kipindupindu bila kuzingatia kanuni za afya.
5: usafirishaji holela wa wagonjwa wa kipindupindu.
6: uandaaji na upikaji chakula bila kuzingatia kanuni za Afya.
                                                                                                 
  Miongoni mwa hatua za msingi katika kujikinga na maambukizi ya kipindupindu, ni kunawa mikono wakati wowote kabla ya kutayarisha au kula chakula, kusafisha vyombo vya chakula baada ya matumizi na kuvihifadhi sehemu safi. Ni muhimu sana kunawa mikono kwa sabuni kwa utaratibu wa kuosha viganja, upande wa nyuma wa mkono, katikati ya vidole na kucha na ufanye hivyo kwa sekunde chache baada ya kwenda haja na kabla ya kula. Lingine ni kuwa na akiba ya maji yaliyochemshwa hususan pasipokuwa na maji safi ya bomba.

Na Salim Gembe
Chanzo cha Habari: Mtandao wa intaneti

No comments:

Post a Comment

Matunda yanayo boresha mfumo wa KINGA YA MWILI

Katika kipindi hiki cha hofu ya corona ni muhimu sana kuhakikisha kinga yako ya mwili iko juu muda wote. Lakini pia ni vizuri katika maisha...