Upungufu wa damu mwilini ni hali
ya mtu kuwa na upungufu wa haemoglobin kwenye mzunguko wa damu tofauti na kiwango
maalum cha kitaalam kulingana na umri na jinsia ya mtu.
Upungufu wa damu mwilini unaweza kugundulika kwa kupima kiwango
cha seli hai nyekundu za damu , yani,
hemoglobin na haematicrit.
Kwa kawaida binadamu anatakiwa kuwa na kiwango maaluma cha damu Kama
ifuatavyo :
UMRI/JINSIA
|
KIWANGO CHA DAMU
|
||
Kabla ya kuzaliwa
(cord blood)
|
13.5- 20.5 (g/dl)
|
||
Siku moja
baada ya kuzaliwa
|
15.0-23.5
(g/dl)
|
||
Miezi6 -
miaka 6
|
11.0 –
14.5 (g/dl)
|
||
Miaka 6 –
miaka 14
|
12.0
-15.5 (g/dl)
|
||
Mtu mzima
mwanamke
|
12.0 –
15.0 (g/dl)
|
||
Mtu mzima
mwanaume
|
13.0 –
17.0 (g/dl)
|
Binadamu ana pokuwa na kiwango tofauti na hiyo au chini ya hivo huwa inamadhara
kwake ,Inapotokea mtu akawa na upungufu hapo ana patiwa matibabu ya visababishi
au kuongezewa damu.
| sawa Pungufu |
VISABABISHI VYA UPUNGUFU WA
DAMU MWILINI
Upungufu wa damu mwilini unaweza kusababishwa na vitu mbali mbali katika
mazingira ya mwanadamu .Visababishi hivi kama;
ü LISHE:hiki ni kisababishi kikuu
katika kuchangia upungufu wa damu katika mwili
wa binadamu. Hii hutokana na kukosa mlo kamili wenye virutubisho maalum katika
kuboresha mzunguko wa damu mwilini,
ü Mfano;
vyakula vyenye madini ya chuma,folic acid, vitamin B,(nyama, mbogamboga,matunda),kukaa
bila kula au kuto kulavizuri,ongezeko la uhitaji wa madini chuma mwilini,. Watu
ambao hula kiasi kidogo cha vyakula vyenye madini chuma hukumbwa sana na tatizohili.
ü MAGONJWA:baadhi ya magonjwa huchangia
pia kwa kiasi kikubwa upungufu wa damu mwilini
haswa magonjwa yale yanayo sambaa au kuenea kwa njia ya damu MFANO;tatizo la figo ,ini,uvimbe au tatizo kwenye mishipa ya damu,kama hook worm , maambukizi ya muda mrefu pia husababisha
mabadiliko au upungufu wa damu mwilini,matatizo
katika seli za damu au kinga za mwli, kutokana na damu nyingi nk.
ü MAGONJWA YA KURITHI: kunabaadhi
ya magonjwa ya kurithi husababisha mtu kuwa rahisikupatatatizo la
upungufuwadamumwilini, kama vile watuwenyematatizokatikaselizadamu au
vichochezivyauzalishajiwadamumwilini (haemoglobinopathies, G-6-P deficiency.nk)
ü
TAKWIMU
YA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI:
Takwim
zinaonesha kuwa wanawake ndio wahanga wakubwa wa tatizohili la upungufu wa damu
mwilini ukilinganisha na wanaume . Pia madhara
ya upungufu wa damu mwilini hutofautiana kulingana na sababu au visababishi
MFANO; kutokwa au kupoteza damu nyingi (80%) hutegemeana na sababu na sehemu damu
inayotoka, kupasuka mishipa ya damu 30-50%, vidonda vya tumbo 1%.
AINA ZA
UPUNGUFU WA DAMU
·
Upungufu wa damu utokanao na lishe
·
Upungufuwa damu utokanao na mabadiliko ya mwili
·
Upungufu wa damu utokanao na magonjwa /maambukizi
DALILI ZA UPUNGUFU WA DAMU MWLINI
| Mkono uliyo kwenye duara una upungufu wa damu |
Watuwengi
huwa na upungufu wa damu mwilini bila kuonesha dalili zozote .Dalili hujitokeza
kulingana na kiwango cha upungufu wa damu na visababishi vyake.
Mtu
mwenye upungufu wa damu mwilini huweza kuonesha dalilizifuatazo;
·
Kujihisi mchovu kupitakiasi bila kufanya shughuli
yoyote
·
Maumivu ya viungo
·
Kushindwakuwa makini katika mambo yako (concentration)
·
Kupumua kwa nguvu au kwa tabu (kupumuaharaka au kubanwanapoumzi)
·
Hali inapokuwa mbaya zaidi mtu huweza kuonesha dalili
za madhara kwenye moyo MFANO; mapigo ya moyo kwenda mbio sana, maumivu ya ghafla
kwenye maeneoya moyo, kukaza na kuuma kwa misuli ya miguuni bila au baada ya kufanya
shughuli. Kukohoa sana,kupumua kwa shida,kutokw
na jasho kupita kiasi,kutokwa na jasho kupita kiasi.
·
Dalili zinazo onekana ni kama kubadilika kwa rangi
ya viganja na macho(vyeupe/njano), vidondamiguuni , kudhoofika na maumivu ya mifupa,
kuvimba haswa miguuni.
MADHARA YA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI
·
Kushindwa kuvumilia mazingira ya baridi (cold intolerance)
·
Upungufu wa hewa safi (oxygen) kwenye viungo mbali
mbali (kutokana na kiwango kidogo kinacho
safirishwa kwenye damu)
·
Kwa mwanamke mjamzito ,hupelekea motto kutokukua vizuri
tumbo ,kuzaa kabla ya mda(njiti) mtoto kufia tumboni ,chupa ya uzazi kupasuka kabla
ya wakati.
·
Kula kwa wingi vyakula vyenye madini chuma. Kama
vile dagaa nyama nk.
·
Kula vyakula vyenye protini kwa wingi kama vile
mayai nyama maziwa nk.
·
Kula mboga mboga mf. Mchicha ,matembele na mboga
zingine
·
Pia kula matunda kwa wingi nk.
N/B
.Kuhakikisha kupata mlo kamili wenye virutubisho vyote, Nakujikinga na maambukizi
ya magonjwa mbali mbali ambayo yanaweza kuwa kichochezi kwa tatizo hili.