Wednesday, 23 October 2019

Lishe bora


Lishe bora
  Lishe bora maana yake ni kula chakula cha kutosha na chakula kinachofaa ili kusaidia mwili kukua vyema ki-afya na mwili kuwa na uwezo wa kupigana na magonjwa. Lishe bora pia husaidia mwili kuwa na nguvu, nguvu ambazo binadamu hutumia kila siku iendayo kwa Mungu katika kuendea majukumu ya kutafuta kipato cha kumfanya aendelee kuishi, hivyo nguvu na maarifa ndiyo vitu vya msingi ki-afya katika shughuli zetu za kila siku. Ili kupata nguvu na afya ya mwili na akili ni lazima ule chakula katika utaratibu unaokubalika yani lishe bora.

 Lishe bora afya madhubuti
 
 Lakini katika maeneo mengi duniani, watu wengi hula chakula cha aina moja ambacho hakina gharama, katika kila mlo. Vyakula hivi ni pamoja na wali, mahindi, mtama, ngano, mihogo, viazi, au ndizi, hii ni kulingana na mazingira ya eneo analo ishi mtu. Ni dhahiri kuwa chakula hiki kikuu kwa kawaida kinasaidia kuupa mwili chakula kinachohitaji kila siku. Lakini hata hivyo, chakula hiki hakikidhi uwezo wa kujenga afya ya mtu. Ili mwili kupata afya nzuri kitahitajika chakula cha ziada kuweza  kusaidia katika kujenga mwili. Vitamini na Madini husaidia kulinda na Kukarabati mwili, na mafuta na sukari humpa binadamu nguvu.

 Chakula cha Lishe bora ni pamoja na, chakula cha protini, matunda na mboga zilizo jaa vitamini na madini. Japo mwanadamu anahitaji kiwango kidogo cha mafuta na sukari.

 




Hivyo ni muhimu kuzingatia kuwa lishe bora ni lazima iwe na vyakula vyenye vyanzo vya :-
 Wanga
mahindi, mpunga, viazi, mihogo, mtama, uwele, ulezi, ngano n.k
Protini
nyama, maziwa, mayai, maharage, karanga n.k
Madini na vitamini
mboga za majani, nyama, maziwa na matunda
Mafuta
maziwa, nyama, mayai, karanga na korosho
Dalili za kukosa lishe bora:

Maumbile: kukonda, mifupa kujitokeza sana, kunyauka, macho kuingia ndani, midomo kukauka, ukavu wa ngozi, nywele kubadilika rangi au kuwa laini sana.
Utendaji kazi: Kupungua kwa uwezo wa kufikiri na kukumbuka mambo muhimu, kuchoka haraka, kushindwa kumaliza kazi kwa muda uliopangwa.
Udhaifu: Kushambuliwa kirahisi na maradhi kama malaria, magonjwa ya ngozi, minyoo, upungufu wa damu mwilini
Ili kuwa na nguvu na afya nzuri inabidi kula mara tatu kwa siku.                                     
 Wataalamu wanatushauri kutumia lishe bora kwa kanuni hii:
Uwiano wa uzito wa mwili = Uzito (kwa kilo)
                                              Kimo (kwa mita)
Lakini ni vizuri zaidi kupata ushauri wa mtaalamu wa afya

Wednesday, 20 March 2019

WAGONJWA WATANO WAPANDIKIZWA FIGO BENJAMIN MKAPA


Na WAMJW – DOM                      

Hospitali ya  Benjamin Mkapa imefanikiwa kupandikiza Figo jumla ya Wagonjwa saba tangu ilipoanza kufanya huduma hiyo kwa kushirikiana na Madaktari kutoka shirika la afya la Tokushukai lilopo nchi ya Japan.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto   wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za kibingwa za magonjwa ya Figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.
Dkt.  Ndugulile amesema kuwa Idadi ya wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 43, ambapo 38 wamepatiwa huduma hiyo kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili na wagonjwa watano(5) hospitali ya Benjamin Mkapa

“Hivi navyoongea tayari mgonjwa mmoja amekwishapandikizwa figo na ameshatoka salama, yupo anaendelea kuangaliwa, lakini wana mpango wa kuwafanyia wengine wawili tutapokuwa tumekamilisha hili tutakuwa na wagonjwa saba ambao wamefanyiwa hospitali hii” alisema Dkt. Ndugulile.
Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kuwa, Serikali imelenga kuhakikisha kwamba inawajengea uwezo Wataalamu wa ndani kufanya upasuaji  wa kibingwa ili waweze kuwahudumia Watanzania bila msaada kutoka Wataalamu wa nje.
“lengo na kusudio ni kuhakikisha kwamba tunajenga uwezo wa ndani wa kuweza kufanya upasuaji huu” Alisema Dkt. Ndugulile
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeokoa zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 4.2 ambacho kingetumika katika matibabu ya wagonjwa 80 mpaka 100 ambao wangepelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
“Wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 42, kama tungewapeleka  wagonjwa nje ya nchi ingegharimu serikali kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kwa idadi hiyo ya wagonjwa.  80 mpaka 100, wakati huduma hii hapa nchini inagharimu kiasi cha shilingi milioni 21 kwa kila mgonjwa.” alisema Dkt. Ndugulile
Aidha, Dkt. Ndugulile amewashukuru Wataalamu kutoka shirika la Tokushukai kutoka nchi ya Japan kwa kujitoa na kuja kuwajengea uwezo Wataalamu wa ndani hali iliyosaidia kupunguza kiasi kikubwa cha fedha ambacho hutumika kwa ajili ya matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje.
“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania nimepita kuwashukuru na kuwapongeza,  kwa sababu badala ya kutusaidia sisi samaki, wenzetu wa Japan wameamua kutupatia sisi mishipi na kutufundisha jinsi ya kujua naamini ujuzi huu utatusaidia sana ” alisema Dkt. Ndugulile.

Wednesday, 6 February 2019

UPUNGUFU WA DAMU MWILINI



 Upungufu wa damu mwilini ni hali ya mtu kuwa na upungufu wa haemoglobin kwenye mzunguko wa damu tofauti na kiwango maalum cha kitaalam kulingana na umri na jinsia ya mtu.
Upungufu wa damu mwilini unaweza kugundulika kwa kupima kiwango cha  seli hai nyekundu za damu , yani, hemoglobin na  haematicrit.
Kwa kawaida binadamu anatakiwa kuwa na kiwango maaluma cha damu Kama ifuatavyo :
                   UMRI/JINSIA
                KIWANGO CHA DAMU
Kabla ya kuzaliwa (cord blood)
 13.5- 20.5 (g/dl)
Siku moja baada ya kuzaliwa
15.0-23.5 (g/dl)
Miezi6  -  miaka 6
11.0 – 14.5 (g/dl)
Miaka 6 – miaka 14
12.0 -15.5 (g/dl)
Mtu mzima mwanamke
Mja mzito
12.0 – 15.0 (g/dl)
11.0 – 14.0 g/dl
Mtu mzima mwanaume
13.0 – 17.0 (g/dl)

Binadamu ana pokuwa na kiwango tofauti na hiyo au chini ya hivo huwa inamadhara kwake ,Inapotokea mtu akawa na upungufu hapo ana patiwa matibabu ya visababishi au kuongezewa damu.
sawa                                        Pungufu


                 VISABABISHI VYA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI
Upungufu wa damu mwilini unaweza kusababishwa na vitu mbali mbali katika mazingira ya mwanadamu .Visababishi hivi kama;

ü  LISHE:hiki ni kisababishi kikuu katika kuchangia upungufu wa damu katika mwili                                                  wa binadamu. Hii hutokana na kukosa mlo kamili wenye virutubisho maalum katika kuboresha mzunguko wa damu mwilini,
ü  Mfano; vyakula vyenye madini ya chuma,folic acid, vitamin B,(nyama, mbogamboga,matunda),kukaa bila kula au kuto kulavizuri,ongezeko la uhitaji wa madini chuma mwilini,. Watu ambao hula kiasi kidogo cha vyakula vyenye madini chuma hukumbwa sana  na tatizohili.
ü  MAGONJWA:baadhi ya magonjwa huchangia pia   kwa kiasi kikubwa upungufu wa damu mwilini haswa magonjwa yale yanayo sambaa au kuenea kwa njia ya damu MFANO;tatizo  la figo ,ini,uvimbe au  tatizo kwenye mishipa ya damu,kama  hook worm , maambukizi ya                           muda mrefu pia husababisha mabadiliko au upungufu wa  damu mwilini,matatizo katika seli za damu au kinga za mwli, kutokana na damu nyingi nk.
ü  MAGONJWA YA KURITHI: kunabaadhi ya magonjwa  ya kurithi husababisha    mtu kuwa rahisikupatatatizo la upungufuwadamumwilini, kama vile watuwenyematatizokatikaselizadamu au vichochezivyauzalishajiwadamumwilini (haemoglobinopathies, G-6-P deficiency.nk)
ü   
TAKWIMU YA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI:

 Takwim zinaonesha kuwa wanawake ndio wahanga wakubwa wa tatizohili la upungufu wa damu mwilini  ukilinganisha na wanaume . Pia madhara ya upungufu wa damu mwilini hutofautiana kulingana na sababu au visababishi MFANO; kutokwa au kupoteza damu nyingi (80%) hutegemeana na sababu na sehemu damu inayotoka, kupasuka mishipa ya damu 30-50%, vidonda vya tumbo 1%.


AINA ZA UPUNGUFU WA DAMU
·         Upungufu wa damu utokanao na lishe
·         Upungufuwa damu utokanao na mabadiliko ya mwili
·         Upungufu wa damu utokanao na magonjwa /maambukizi


DALILI ZA UPUNGUFU WA DAMU MWLINI
Mkono uliyo kwenye duara una upungufu wa damu


Watuwengi huwa na upungufu wa damu mwilini bila kuonesha dalili zozote .Dalili hujitokeza kulingana na kiwango cha upungufu wa damu na visababishi vyake.
Mtu mwenye upungufu wa damu mwilini huweza kuonesha dalilizifuatazo;

·         Kujihisi mchovu kupitakiasi bila kufanya shughuli yoyote
·         Maumivu ya viungo
·         Kushindwakuwa makini katika mambo yako (concentration)
·         Kupumua kwa nguvu au kwa tabu (kupumuaharaka au kubanwanapoumzi)
·         Hali inapokuwa mbaya zaidi mtu huweza kuonesha dalili za madhara kwenye moyo MFANO; mapigo ya moyo kwenda mbio sana, maumivu ya ghafla kwenye maeneoya moyo, kukaza na kuuma kwa misuli ya miguuni bila au baada ya kufanya shughuli.  Kukohoa sana,kupumua kwa shida,kutokw na jasho kupita kiasi,kutokwa na jasho kupita kiasi.
·         Dalili zinazo onekana ni kama kubadilika kwa rangi ya viganja na macho(vyeupe/njano), vidondamiguuni , kudhoofika na maumivu ya mifupa, kuvimba haswa miguuni.
            MADHARA YA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI
·         Kushindwa kuvumilia mazingira ya baridi (cold intolerance)
·         Upungufu wa hewa safi (oxygen) kwenye viungo mbali mbali (kutokana na kiwango kidogo kinacho safirishwa kwenye damu)
·         Kwa mwanamke mjamzito ,hupelekea motto kutokukua vizuri tumbo ,kuzaa kabla ya mda(njiti) mtoto kufia tumboni ,chupa ya uzazi kupasuka kabla ya wakati.
JINSI YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI.
·         Kula kwa wingi vyakula vyenye madini chuma. Kama vile dagaa nyama nk.
·         Kula vyakula vyenye protini kwa wingi kama vile mayai nyama maziwa nk.
·         Kula mboga mboga mf. Mchicha ,matembele na mboga zingine
·         Pia kula matunda kwa wingi nk.

N/B .Kuhakikisha kupata mlo kamili wenye virutubisho vyote, Nakujikinga na maambukizi ya magonjwa mbali mbali ambayo yanaweza kuwa kichochezi kwa tatizo hili.

Matunda yanayo boresha mfumo wa KINGA YA MWILI

Katika kipindi hiki cha hofu ya corona ni muhimu sana kuhakikisha kinga yako ya mwili iko juu muda wote. Lakini pia ni vizuri katika maisha...