Thursday, 21 June 2018

HOMA YA UZAZI



Homa ya uzazi ni homa ambayo hutokea kwa mwanamke wiki sita baada ya kujifungua,hali hii pia huweza kutokea kwa mwanamke alie jifungua kwa njia yoyote ya kawaida au upasuaji,pia hutokea wakati wa kunyonyesha. Homa ya uzazi inaweza kuwa ni maambukizi kwenye sehemu ya maji ya uzazi au maambukizi kwenye mji  wa mimba yani (endometritis) pia huweza kuwa ni homa yoyote baada au wakati wa kujifungua. Visababishi vya Homa ya uzazi vinaweza kuwa kwasababu ya maambukizi au wakati mwingine si kwa sababu ya maambukizi . Upande wa  Maambukizi ambayo hutokea wakati wa kipindi cha uzazi dalili zake kubwa ni homa lakini jambo la kutiliwa maanani hapa ni kwamba sio kila homa inayotokea wakati wa uzazi ni kwa sababu ya maambukizi, bali wakati mwengine huwa ni kawaida mzazi kupata homa wakati wa uzazi.
 Mwanamke anapopata homa wakati wa uzazi, maranyingi huashiria maambukizi kwenye maji ya uzazi,maambukizi kwenye mji wa mimda,maambukizi kwenye kidonda kwa wale waliozaa kwa njia ya upasuaji,maambukizi kwenye matiti, maambukizi ya kwenye kidonda ukeni kwa wale waliongezewa njia, maambukizi  kwenye mfumo wa upumuaji/hewa, mabaki ya uchafu tumboni maambukizi kwenye mfumo wa mkojo (UTI), pia matatizo ya upumuaji yatokanayo na dawa za usingizi kwa wale walio jifungua kwa njia ya upasuaji.

Madhara yatokanayo na homa ya uzazi

  Homa ya uzazi ni moja ya sababu  kubwa za magonjwa na vifo kwa wakina mama walio jifingua hapa Tanzania. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia,wazee na watoto inakadiriwa kuwa asilimia 11% ya vifo vya uzazi husababishwa na homa ya uzazi.Katika hali hii mama hufa kutokana na maambukizi.

Visababishi vya homa ya uzazi

Homa ya uzazi inaweza kusababishwa kutokana na sababu mbalimbali. Miongoni mwa  sababu ambazo husababisha homa ya uzazi ni pamoja na kufanya vipimo vya njia ya uzazi mara nyingi isivyo kawaida,uchungu wa mda mrefu au kutofunguka kwa njia, chupa ya uzazi kupasuka kabla ya wakati au kupasuliwa mapema, sababu nyingine ni kuzaa kabla ya mda (miezi tisa) au kuzaa njiti,kuzaa kwa msaada wa kuongezewa njia au kuzalishwa na vifaa vya kusaidia kuzalisha, kubakia kwa uchafu wa uzazi tumboni, usafi wa mama binafsi,magonjwa  ya zinaa kwa mama,na upungufu wa damu wakati wa ujauzito.

Dalili atakazo onesha mama mwenye homa ya uzazi

 Miongoni mwa dalili za Mama mwenye homa ya uzazi ni pamoja na Joto la mwili kuwa juu  kati ya  degiri thelathini na nane au zaidi, Maumivu ya tumbo la chini, Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya ukeni, kondo la uzazi kuchelewa kupotea au kuwa na maumivu, Majipu au kuvimba kwenye nyonga kutokwa na damu ukeni.

Jinsi ya kuzuia homa ya uzazi

 Homa ya uzazi huweza kuzuiwa kwa Kuzingatia usafi wakati wa kuzalisha na baada ya kujifungua,kupunguza idadi ya vipimo vya njia ya uzazi kwa mama, kuzuia au kutokupasua chupa ya uzazi mapema , Kupunguza muda wa uchungu kwa kutumia chati maalum au mazoezi kwa mama, huduma maalum zitolewazo kwaajili ya uchungu ni muhimu, ni muhimu pia mama kujitahidi usafi baada ya kujifungua.
By
Maunda Salim Gembe                                                                                                                                                                 Nuru ya siha project

 

Vyanzo vya habari:
-Baker,P.&Monga, A.(2006). Obstratrics by Ten Teachers (18th ED). London: Hodder Arnold.
-Oats, .J., Abraham, S.(2005) Llewellyn-Jones Fundamental of Obstetrics and Gynaecology. (8th Ed).Edinburgh:Mosby.
-DeCherney,A.H.&Nathan,L.(2002)Current Obstetrics and Gynaecology (9th Ed).McGraw Hill.
ACCESS MEDICAL & DIALYSIS CENTER
H.H MUSSA
0715 620245


Matunda yanayo boresha mfumo wa KINGA YA MWILI

Katika kipindi hiki cha hofu ya corona ni muhimu sana kuhakikisha kinga yako ya mwili iko juu muda wote. Lakini pia ni vizuri katika maisha...