Kula chakula chenye
virutubisho sahihi ni jukumu la lazima la binadamu ili kuwa na afya njema.
Dunia ina vyakula vya asili ambavyo ndani yake kuna virutubisho muhimu
vinavyosaidia mwili kupambana na magonjwa na pia kuimarisha afya. Vyakula hivyo
ni vile vya kijani ambavyo vina uwezo mkubwa zaidi katika kuponya magonjwa na
kusaidia pia kukarabati, kujenga mwili na kuimarisha siha.
Ngozi nayo ni sehemu
muhimu ya mwili ambayo ina jukumu kubwa la kuukinga na kuufunika mwili na
viungo mbalimbali na afya yake ni jambo la kuzingatiwa. Aina za vyakula
tunavyopendelea kula vinaweza kuchangia katika muonekano wa ngozi zetu.
Kuna aina za vyakula
vinavyosaidia katika kutunza ngozi yako bila gharama kubwa. Bi Samatha Heller
mtaalamu wa lishe katika Chuo Kikuu cha Tiba cha New York City anasema kuwa,
kila tunachokula kinakuwa sehemu ya mwili wetu na kila tunapo vyakula bora
ndivyo ngozi zinavyoonekana vizuri. Naye Elein Linker mtaalamu wa biokemikali
na mwasisi wa kituo cha kutunza ngozi cha DDF anasema, matatizo mengi ya ngozi
kama vile chunusi ya aczema (ngozi kuwa
nyekundu,kuvimba,kuwasha au ukavu) itching and dryness yanaweza kuwa yanahusiana na lishe. Hivyo
tunashauriwa kujitahidi kufuata kanuni za afya ili kuufanya mwili uwe na afya
nzuri kwa kula chakula bora, kufanya mazoezi, kupumzika kwa muda mrefu, vivyo
hivyo ngozi nayo inatakiwa kutunzwa vyema kupitia lishe.
Asali ambayo hutengenezwa na nyuki kwa
viambato asilia ni chakula muhimu kwa ajili ya kuimarisha afya ya ngozi na pia
afya ya binadamu. Sababu kubwa ya kutumia mafuta ya kuipaka ni kuifanya ngozi
iwe na unyevu nyevu. Asali husaidia kutunza na kuhifadhi unyevu kwenye ngozi na
ina kiwango kikubwa cha sukari na asidi ambazo huzuia vijidudu wanaozaliana
kwenye ngozi. Vyakula vingi vya baharini pia vina kiwango kikubwa cha Zinc na
Omega 3 ambazo ni muhimu kwa siha ya ngozi. Faida za Omega 3 ni pamoja na
kuondoa kukakamaa au ukavu wa ngozi, kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi
na husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha ngozi.
Kiini cha yai kina
vitamini A na B huku sehemu yenye ute ikiwa na protini nyingi ambayo ni muhimu
pia kwa ngozi . Mada ya Tretinoin inayopatikana kwenye Vitamin A husaidia
kuondoa chunusi na mikunjo ya ngozi. Mada nyingine ya Biotin inayopatikana
kwenye Vitamin B ni muhimu kwa afya ya ngozi na kucha na protini inayopatikana
kwenye ute wa yai ni muhimu katika kuifanya ngozi iwe nyororo na yenye kung'aa na
pia husaidia ngozi kujilinda vizuri na mionzi ya jua.
Matunda yenye
vitamini C kama vile chungwa, limao na mengineyo ni muhimu pia katika
kuimarisha afya ya ngozi, kwa sababu husaida kutengeneza collagen, ambayo ni
aina ya protini inayotengeneza ngozi. Vitamini C inasaidia kuondoa uvimbe na
mikunjo ya ngozi na hivyo kuilinda ngozi isizeeke mapema.
Mboga za majani pia ni muhimu kwa afya ya ngozi kama
tujuavyo zimesheheni vitamin na virutubisho vya aina mbalimbali vyenye faida
kubwa kwa ngozi na mwili kwa ujumla.
Chanzo cha habari:
Mitandao


