Wednesday, 23 October 2019

Lishe bora


Lishe bora
  Lishe bora maana yake ni kula chakula cha kutosha na chakula kinachofaa ili kusaidia mwili kukua vyema ki-afya na mwili kuwa na uwezo wa kupigana na magonjwa. Lishe bora pia husaidia mwili kuwa na nguvu, nguvu ambazo binadamu hutumia kila siku iendayo kwa Mungu katika kuendea majukumu ya kutafuta kipato cha kumfanya aendelee kuishi, hivyo nguvu na maarifa ndiyo vitu vya msingi ki-afya katika shughuli zetu za kila siku. Ili kupata nguvu na afya ya mwili na akili ni lazima ule chakula katika utaratibu unaokubalika yani lishe bora.

 Lishe bora afya madhubuti
 
 Lakini katika maeneo mengi duniani, watu wengi hula chakula cha aina moja ambacho hakina gharama, katika kila mlo. Vyakula hivi ni pamoja na wali, mahindi, mtama, ngano, mihogo, viazi, au ndizi, hii ni kulingana na mazingira ya eneo analo ishi mtu. Ni dhahiri kuwa chakula hiki kikuu kwa kawaida kinasaidia kuupa mwili chakula kinachohitaji kila siku. Lakini hata hivyo, chakula hiki hakikidhi uwezo wa kujenga afya ya mtu. Ili mwili kupata afya nzuri kitahitajika chakula cha ziada kuweza  kusaidia katika kujenga mwili. Vitamini na Madini husaidia kulinda na Kukarabati mwili, na mafuta na sukari humpa binadamu nguvu.

 Chakula cha Lishe bora ni pamoja na, chakula cha protini, matunda na mboga zilizo jaa vitamini na madini. Japo mwanadamu anahitaji kiwango kidogo cha mafuta na sukari.

 




Hivyo ni muhimu kuzingatia kuwa lishe bora ni lazima iwe na vyakula vyenye vyanzo vya :-
 Wanga
mahindi, mpunga, viazi, mihogo, mtama, uwele, ulezi, ngano n.k
Protini
nyama, maziwa, mayai, maharage, karanga n.k
Madini na vitamini
mboga za majani, nyama, maziwa na matunda
Mafuta
maziwa, nyama, mayai, karanga na korosho
Dalili za kukosa lishe bora:

Maumbile: kukonda, mifupa kujitokeza sana, kunyauka, macho kuingia ndani, midomo kukauka, ukavu wa ngozi, nywele kubadilika rangi au kuwa laini sana.
Utendaji kazi: Kupungua kwa uwezo wa kufikiri na kukumbuka mambo muhimu, kuchoka haraka, kushindwa kumaliza kazi kwa muda uliopangwa.
Udhaifu: Kushambuliwa kirahisi na maradhi kama malaria, magonjwa ya ngozi, minyoo, upungufu wa damu mwilini
Ili kuwa na nguvu na afya nzuri inabidi kula mara tatu kwa siku.                                     
 Wataalamu wanatushauri kutumia lishe bora kwa kanuni hii:
Uwiano wa uzito wa mwili = Uzito (kwa kilo)
                                              Kimo (kwa mita)
Lakini ni vizuri zaidi kupata ushauri wa mtaalamu wa afya

Matunda yanayo boresha mfumo wa KINGA YA MWILI

Katika kipindi hiki cha hofu ya corona ni muhimu sana kuhakikisha kinga yako ya mwili iko juu muda wote. Lakini pia ni vizuri katika maisha...