Thursday, 21 June 2018

HOMA YA UZAZI



Homa ya uzazi ni homa ambayo hutokea kwa mwanamke wiki sita baada ya kujifungua,hali hii pia huweza kutokea kwa mwanamke alie jifungua kwa njia yoyote ya kawaida au upasuaji,pia hutokea wakati wa kunyonyesha. Homa ya uzazi inaweza kuwa ni maambukizi kwenye sehemu ya maji ya uzazi au maambukizi kwenye mji  wa mimba yani (endometritis) pia huweza kuwa ni homa yoyote baada au wakati wa kujifungua. Visababishi vya Homa ya uzazi vinaweza kuwa kwasababu ya maambukizi au wakati mwingine si kwa sababu ya maambukizi . Upande wa  Maambukizi ambayo hutokea wakati wa kipindi cha uzazi dalili zake kubwa ni homa lakini jambo la kutiliwa maanani hapa ni kwamba sio kila homa inayotokea wakati wa uzazi ni kwa sababu ya maambukizi, bali wakati mwengine huwa ni kawaida mzazi kupata homa wakati wa uzazi.
 Mwanamke anapopata homa wakati wa uzazi, maranyingi huashiria maambukizi kwenye maji ya uzazi,maambukizi kwenye mji wa mimda,maambukizi kwenye kidonda kwa wale waliozaa kwa njia ya upasuaji,maambukizi kwenye matiti, maambukizi ya kwenye kidonda ukeni kwa wale waliongezewa njia, maambukizi  kwenye mfumo wa upumuaji/hewa, mabaki ya uchafu tumboni maambukizi kwenye mfumo wa mkojo (UTI), pia matatizo ya upumuaji yatokanayo na dawa za usingizi kwa wale walio jifungua kwa njia ya upasuaji.

Madhara yatokanayo na homa ya uzazi

  Homa ya uzazi ni moja ya sababu  kubwa za magonjwa na vifo kwa wakina mama walio jifingua hapa Tanzania. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia,wazee na watoto inakadiriwa kuwa asilimia 11% ya vifo vya uzazi husababishwa na homa ya uzazi.Katika hali hii mama hufa kutokana na maambukizi.

Visababishi vya homa ya uzazi

Homa ya uzazi inaweza kusababishwa kutokana na sababu mbalimbali. Miongoni mwa  sababu ambazo husababisha homa ya uzazi ni pamoja na kufanya vipimo vya njia ya uzazi mara nyingi isivyo kawaida,uchungu wa mda mrefu au kutofunguka kwa njia, chupa ya uzazi kupasuka kabla ya wakati au kupasuliwa mapema, sababu nyingine ni kuzaa kabla ya mda (miezi tisa) au kuzaa njiti,kuzaa kwa msaada wa kuongezewa njia au kuzalishwa na vifaa vya kusaidia kuzalisha, kubakia kwa uchafu wa uzazi tumboni, usafi wa mama binafsi,magonjwa  ya zinaa kwa mama,na upungufu wa damu wakati wa ujauzito.

Dalili atakazo onesha mama mwenye homa ya uzazi

 Miongoni mwa dalili za Mama mwenye homa ya uzazi ni pamoja na Joto la mwili kuwa juu  kati ya  degiri thelathini na nane au zaidi, Maumivu ya tumbo la chini, Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya ukeni, kondo la uzazi kuchelewa kupotea au kuwa na maumivu, Majipu au kuvimba kwenye nyonga kutokwa na damu ukeni.

Jinsi ya kuzuia homa ya uzazi

 Homa ya uzazi huweza kuzuiwa kwa Kuzingatia usafi wakati wa kuzalisha na baada ya kujifungua,kupunguza idadi ya vipimo vya njia ya uzazi kwa mama, kuzuia au kutokupasua chupa ya uzazi mapema , Kupunguza muda wa uchungu kwa kutumia chati maalum au mazoezi kwa mama, huduma maalum zitolewazo kwaajili ya uchungu ni muhimu, ni muhimu pia mama kujitahidi usafi baada ya kujifungua.
By
Maunda Salim Gembe                                                                                                                                                                 Nuru ya siha project

 

Vyanzo vya habari:
-Baker,P.&Monga, A.(2006). Obstratrics by Ten Teachers (18th ED). London: Hodder Arnold.
-Oats, .J., Abraham, S.(2005) Llewellyn-Jones Fundamental of Obstetrics and Gynaecology. (8th Ed).Edinburgh:Mosby.
-DeCherney,A.H.&Nathan,L.(2002)Current Obstetrics and Gynaecology (9th Ed).McGraw Hill.
ACCESS MEDICAL & DIALYSIS CENTER
H.H MUSSA
0715 620245


Tuesday, 13 February 2018

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha



 Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, mwili wako unahitaji virutubishi ili kusaidia ukuaji wa mwili, kama ni kijana mwili wako una mahitaji maalumu unayoyahitajia kudhamini makuzi ya kiafya ya mwili wako wakati wa utu uzima na wakati unapokuwa mtu mzima unahitaji kuwa na uzito uliolingana na mwili wa wastani.
Tukiangalia katika upande wa Akina mama wajawazito na wale wanaonyonyesha nao pia wana vyakula vyao maalumu wanavyohitajia tofauti kabisa na wanawake wengine. Uchunguzi wa kitiba uliofanywa unaonyesha kuwa, hali ya kiafya ya mama mjazito huwa na athari mbalimbali kwa mtoto atakayezaliwa. Vile vile kuna ushahidi mkubwa kuwa magonjwa sugu ya watu wazima huanzia wakati mtoto bado akiwa tumboni mwa mama yake akiwa katika hali ya kiluilui au (foetus). Kwa hivyo akina mama wajawazito wanashauriwa kuzingatia vyakula wanavyokula kabla na baada ya kushika mimba.  
Sasa tuangalie athari za chakula kwa afya ya mtoto na virutubisho vinavyopaswa kujumuishwa katika mlo wa mama mjamzito. Chakula cha mama mjamzito kinaweza kuwa na athari kubwa muhimu kwa afya ya watoto kwa miaka mingi baada ya kuzaliwa. Miaka kadhaa ya hivi karibuni, Jarida la Masuala ya Lishe la Uingereza la Prestigious lilichapisha makala tatu kuhusu athari za lishe ya mama mjamzito kwa afya na ukuaji wa kiakili wa mtoto ambaye bado hajazaliwa. Wengi wanafahamu kuwa akina mama wajawazito wanapaswa kula chakula chenye virutubisho vyote vinavyohitajika ili kuhakikisha kuwa watoto wao watakaowazaa wamerutibika vya kutosha wakati wakiwa kwenye fuko la uzazi. Hata hivyo, kile ambacho hatukubaliani nacho hivi sasa ni kwamba chakula cha mama mwenye mimba kinaweza kuwa na taathira chanya kwa afya ya watoto kwa muda wa miaka mingi, baada ya kuzaliwa. Hivi sasa imethibitika kuwa kile kinacholiwa na akina mama wakati wa ujauzito, chakula ambacho kitakuwa kimejumuisha virutubisho vyote vinavyotakiwa, kinaweza kuwafanya watoto wao watakaozaliwa kuwa werevu zaidi. Kwani wataalamu wa afya wanasema kuwa hivi sasa wanaweza kuandaa kizazi kipya cha watoto werevu kwa kula chakula kinachotakikana wakati wa ujauzito. Akina mama wajawazito ambao katika kipindi cha ujauzito hawakupata lishe bora isiyo na mada za protini, nishati, madini na vitamini kwa ujumla huzaa watoto walio na uzito wa chini. Aidha watoto hao huwa na uwezekano mkubwa wa kukumbuwa na magonjwa ya kisukari katika kipindi cha utu uzima.
Wapenzi wasikilizaji baada ya kufahamu umuhimu wa kula lishe bora kwa mama mjamzito na athari zake chanya kwa mtoto atakayezaliwa, sasa tuangalie hatari ya unywaji pombe kwa akinamama wajawazito. Watu wengi wanafahamu madhara yanayotokana na utumiaji wa madawa ya kulevya na ya kawaida pamoja na uvutaji sigara wakati wa ujauzito, lakini wanawake wengi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu madhara yanayosababishwa na unywaji pombe wakati wa ujauzito. Utasikia mume au ndugu, jamaa na marafiki wakimshawishi mama mjamzito kwa maneno kama vile" hebu pata kinywaji, kitakuburidisha, kunywa mvinyo kidogo tusherehekee mimba yako. Chupa moja haiwezi kukuathiri bali itakusisimua tu, Hebu tusherehekee sikukuu" n.k. Nadhani wengi tumewahi kusikia maneno kama haya na ushauri usiofaa ambao hauna faida yoyote ghairi ya kuandaa madhara kwa mtoto atakayezaliwa.
Athari za pombe kwa mtoto ambaye bado hajazaliwa:
Unywaji pombe wa aina zozote wakati mama akiwa na mimba huwa na madhara tofauti kwa mtoto aliye tumboni mwake, kuanzia zile za wastani hadi kubwa. Kumbuka kuwa mama anapokunywa pombe mtoto naye hunywa pia. Kuna madhara makuu matatu yanayoweza kumsibu mtoto ambaye bado hajazaliwa iwapo mama yake alikuwa akinywa pombe wakati wa ujauzito. Mosi, ni kuweko hatari kubwa ya kutoka mimba au kuzaliwa mtoto kabla ya miezi tisa, pili, chembe za mwili za mtoto aliye tumboni zinaweza kuathiriwa au anaweza kuwa na uzito mdogo na kuzaliwa akiwa na ulemavu zaidi ya mmoja., tatu, chembe za ubongo wa mtoto huyo zinaweza kuharibiwa na pombe na mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ambayo kitaalamu hujulikana kama Foetal alcohol syndrome. Miongoni mwa madhara yanayoweza kumpata mtoto ni kama vile kuzaliwa akiwa na ulemabu wa kimwili na kiakili. Kwa upande wa kimwili, mtoto huweza kuathiriwa na mtindio wa ubongo au brain retardation, mtoto anaweza kuzaliwa akiwa na kichwa kidogo sana, na uso wake kuwa na mwanya mkubwa baina ya pua na mdomo. Kwa upande wa macho, wengine huzaliwa wakiwa na matatizo ya kuona, masikio hushambuliwa na baadhi ya magonjwa, n.k.. Na tukitazama upande wa ukuaji wa kimaanawi wa mtoto, kuna mambo kadha wa kadha ambayo mama anaweza kuyafanya ili kuandaa misingi bora ya kuwa Muislamu mwema. Maimamu watukufu wametuambia kuwa, mama mjamzito anapasa daima kuwa katika hali ya wudhu. Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma anapendelea kumuona mja wake akiwa katika wudhu huku malaika wakimzunguka. Hivyo mama hushauriwa kujiepusha na kutenda dhambi, kwa sababu jambo hilo litakuwa na athari ya moja kwa moja kwa shakhsiya ya mtoto. Kwa hivyo ni jambo lenye umuhimu kwa akina mama kuwaandalia watoto wetu mwanzo mzuri wa makuzi bora tangu wakiwa tumboni.
Na sasa hebu tuangalie jinsi unene unavyosababisha hatari kubwa ya saratani ya matiti kwa wanawake. Wanawake wanaoongezeka uzito kupita kiasi katika utu uzima, wanakabiliwa na hatari kubwa na ya muda mrefu ya kukumbwa na saratani za matiti. Uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa, uzito na kansa ya matiti vinaweza kuwa na uhusiano wa karibu. Utafiti uliofanywa kwa akinamama zaidi ya elfu 44 nchini Marekani umeonyesha kuwa, kadiri mwanamke anavyozidi kunenepa, ndivyo anavyozidi kujiweka katika hatari ya kukumbwa na kansa mbalimbali, tena katika hatua zake zote. Hatari ya saratani ya matiti imehusishwa na ongezeko la viwango vya hormone ya estrogen na tishu za mafuta zinazozalisha hormone hiyo. Hivyo basi, akina mama wanashauriwa kuboresha uzito wa mwili kwa kufuata misingi ya afya katika kipindi chote cha utu uzima. 

Tuesday, 6 February 2018

THE 9TH CONGRESS OF AFRICAN SOCIETY FOR BLOOD TRANSFUSION



1st Announcement
The African Society for Blood Transfusion (AfSBT) in collaboration with the Tanzania National Blood Transfusion Services announces the 09th Edition of its Biennial Scientific Congress, taking place at The Tanzania Convention Centre in Arusha, United Republic of Tanzania from 19 to 22 June 2018. The Congress is running under the theme:
Reducing Maternal and New Born Mortality: The role of safe blood Transfusion”
The Congress is held in a different African country, every two years with the host country alternating between Anglophone and Francophone countries, and brings together world experts in the blood banking, policymakers and other key stakeholders who all have a role to play in the field of transfusion medicine. The Arusha 2018 Congress is expected to be attended by more than 350 delegates and shall be the ideal setting to renew friendships, make acquaintances, network with other professionals in the field, present their work and also find some time to visit the wonders of this beautiful country.
The Tanzania Convention Centre (TCC)
Located at the heart of Africa, midway between Cairo and Cape Town, lying in the outskirts of the Arusha City, The Tanzania Convention Centre (TCC) is a perfect venue for meeting requirements, and has a long lived best image in hosting international conferences and events in Tanzania and in the region as a whole
Accommodation:
The official Hotel for the 09th Congress of the African Society for Blood Transfusion is the Ngurdoto Mountain Lodge. Within the same compound as the Tanzania Convention Centre, nestled between Mount Meru and Mount Kilimanjaro, the Ngurdoto Mountain Lodge is located within a lush coffee plantation stretching over 140 acres, with natural streams flowing from Mount Meru passing through the property. The flourishing vegetation and magnificent views of the snow-capped Mt Kilimanjaro and the towering Mount Meru, right in front of the lodge, is an absolutely awesome sight. This lodge is ideally located between Arusha town and Kilimanjaro International Airport, 27 km either way. The lodge has about 350 rooms ranging from presidential suites, executive cottages, deluxe and standard rooms.
For more information, brochure and inscriptions contact:
The Congress Secretariat
Shades of Green Congresses Ltd
East African Community Road, AICC Complex, Ngorongoro Building, 06th Floor
P.O. Box 12554, Arusha, Tanzania
Phone: +255 27 2050081| +255 27 2050082-Fax: +255 27 2050083
Email: afsbt2018@shadesofgreencongresses.com

Thursday, 18 January 2018

Ugonjwa wa Kipindupindu



 Kipindupindu ni miongoni mwa magonjwa ambayo husababishwa na aina ya bakteria aitwaye Vibrio cholerae, bacteria huyu husababisha mtu kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya mchele. Ugonjwa huu ni wa kuambukizwa kwa njia ya viini vinavyoenezwa kupitia maji yaliyo changanyika na  kinyesi au matapishi kutoka kwa wagonjwa wenye Kipindupindu. Mlundikano wa taka na maji machafu ni moingoni mwa vyanzo vya maambukizi ya Kipindupindu.


Mlundikano wa Taka kwenye maeneo ya wapita njia

Aidha matumizi ya choo yasiyo sahihi pia huchangia maambukizi ya ugonjwa huu. Kwa mujibu wa taarifa za ya idara ya huduma za Afya na usafi wa mazingira Wizara ya Afya kipindupindu huenea kwa njia kuu sita:
1: kutokunawa mikono kwa maji safi na salama yanayotiririka na sabuni kabla ya kula au baada ya kutoka chooni.
2:kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salama.
3: kunywa maji yasiyosafi na salama.
4:kumhudumia mgonjwa mwenye dalili za kipindupindu bila kuzingatia kanuni za afya.
5: usafirishaji holela wa wagonjwa wa kipindupindu.
6: uandaaji na upikaji chakula bila kuzingatia kanuni za Afya.
                                                                                                 
  Miongoni mwa hatua za msingi katika kujikinga na maambukizi ya kipindupindu, ni kunawa mikono wakati wowote kabla ya kutayarisha au kula chakula, kusafisha vyombo vya chakula baada ya matumizi na kuvihifadhi sehemu safi. Ni muhimu sana kunawa mikono kwa sabuni kwa utaratibu wa kuosha viganja, upande wa nyuma wa mkono, katikati ya vidole na kucha na ufanye hivyo kwa sekunde chache baada ya kwenda haja na kabla ya kula. Lingine ni kuwa na akiba ya maji yaliyochemshwa hususan pasipokuwa na maji safi ya bomba.

Na Salim Gembe
Chanzo cha Habari: Mtandao wa intaneti

Matunda yanayo boresha mfumo wa KINGA YA MWILI

Katika kipindi hiki cha hofu ya corona ni muhimu sana kuhakikisha kinga yako ya mwili iko juu muda wote. Lakini pia ni vizuri katika maisha...