Unga wa dona kwa mchicha...
Kila Mtu
anaweza kula chakula bora!
Ugali wa dona na mchicha ni maandalizi ya chakula cha bei
nafuu mno…lakini ni miongoni mwa chakula bora.
Unga wa dona ulioandaliwa vizuri huwa una faida nyingi sana
zaidi ya hata unga ambao umekobolewa. Faida hizo ni za kiuchumi au hata za
kiafya.
Faida ya Matumizi ya Unga
wa dona
Kiuchumi:
1.
Ukisaga mahindi bila ya kukoboa unapata unga
mwingi kwa kila kilo utakayoisaga. Hii ni kwa sababu ukoboaji wa mahindi
kunapoteza kiasi fulani cha unga na virutubisho pia.
2. Uandaaji wa
mapishi ya unga wa dona ni rahisi zaidi katika ngazi ya familia.
Kiafya:
Katika Unga wa dona kuna kiasi kikubwa cha mafuta, protini, madini, vitamini, na nyuzinyuzi (fibre). Kwahiyo, unaimarisha zaidi lishe ya mlaji.
Faida za
kula Mchicha(Kwa uchache)
1.
Huboresha mfumo wa Kinga mwili
2.
Huboresha uwezo wa kuona
3.
Huboresha mfumo wa akili na nevu (nervous
system)

