Lishe bora
Lishe bora maana yake ni kula
chakula cha kutosha na chakula kinachofaa ili kusaidia mwili kukua vyema
ki-afya na mwili kuwa na uwezo wa kupigana na magonjwa. Lishe bora pia husaidia
mwili kuwa na nguvu, nguvu ambazo binadamu hutumia kila siku iendayo kwa Mungu
katika kuendea majukumu ya kutafuta kipato cha kumfanya aendelee kuishi, hivyo nguvu na maarifa ndiyo vitu vya msingi ki-afya katika
shughuli zetu za kila siku. Ili kupata nguvu na afya ya mwili na akili ni
lazima ule chakula katika utaratibu unaokubalika yani lishe bora.

Lishe bora afya madhubuti
Lakini katika maeneo mengi duniani, watu wengi
hula chakula cha aina moja ambacho hakina gharama, katika kila mlo. Vyakula
hivi ni pamoja na wali, mahindi, mtama, ngano, mihogo, viazi, au ndizi, hii ni
kulingana na mazingira ya eneo analo ishi mtu. Ni dhahiri kuwa chakula hiki
kikuu kwa kawaida kinasaidia kuupa mwili chakula kinachohitaji kila siku. Lakini
hata hivyo, chakula hiki hakikidhi uwezo wa kujenga afya ya mtu. Ili mwili
kupata afya nzuri kitahitajika chakula cha ziada kuweza kusaidia katika kujenga mwili. Vitamini na
Madini husaidia kulinda na Kukarabati mwili, na mafuta na sukari humpa binadamu
nguvu.
Chakula cha Lishe bora ni pamoja na, chakula cha protini, matunda na mboga zilizo jaa vitamini na madini. Japo mwanadamu anahitaji kiwango kidogo cha mafuta na sukari.
Chakula cha Lishe bora ni pamoja na, chakula cha protini, matunda na mboga zilizo jaa vitamini na madini. Japo mwanadamu anahitaji kiwango kidogo cha mafuta na sukari.
Hivyo ni muhimu kuzingatia kuwa
lishe bora ni lazima iwe na vyakula vyenye vyanzo vya :-
|
Wanga
|
mahindi, mpunga, viazi, mihogo,
mtama, uwele, ulezi, ngano n.k
|
|
Protini
|
nyama, maziwa, mayai, maharage,
karanga n.k
|
|
Madini na vitamini
|
mboga za majani, nyama, maziwa na
matunda
|
|
Mafuta
|
maziwa, nyama, mayai, karanga na
korosho
|
Dalili za kukosa lishe bora:
Maumbile: kukonda, mifupa kujitokeza sana, kunyauka, macho kuingia
ndani, midomo kukauka, ukavu wa ngozi, nywele kubadilika rangi au kuwa laini
sana.
Utendaji kazi: Kupungua kwa uwezo wa kufikiri na kukumbuka mambo muhimu,
kuchoka haraka, kushindwa kumaliza kazi kwa muda uliopangwa.
Udhaifu: Kushambuliwa
kirahisi na maradhi kama malaria, magonjwa ya ngozi, minyoo, upungufu wa damu
mwilini
Ili kuwa na nguvu na afya nzuri
inabidi kula mara tatu kwa siku.
Wataalamu wanatushauri
kutumia lishe bora kwa kanuni hii:
Uwiano wa uzito wa mwili = Uzito
(kwa kilo)
Kimo (kwa mita)
Kimo (kwa mita)
Lakini ni vizuri zaidi kupata
ushauri wa mtaalamu wa afya

No comments:
Post a Comment